kwamamaza 7

Zimbabwe:Raia wa marekani ashtakiwa kutaka kipindua serikali ya Mugabe

0

Raia mmoja wa Marekani Bi Martha O’Donovan’ mwenye umri wa miaka 25 amefikishwa mahakamani huko mjini Harare ambako anakabiliwa na kosa kuu la madai ya kujaribu kuipindua serikali ya Rais Mugabe.

Adhabu ya kosa hilo kwa anayepatikana na hatia ni kifungo cha miaka 20 jela.

Police wanamtuhumu kwamba ndiye anayendesha akaunti ya Twitter iitwayo @matigary ambapo muliwekwa maandishi ya kuhujumu na kumkosea heshima rais Robert Mugabe.

Baadhi ya maandishi yaliyo kwenye akaunti hiyo yanasema yafuatayo ”Nchi yaongozwa na mzee mgonjwa mwenye ubinafsi mkubwa”.

Bi O’Donovan -ambaye huendesha mtandao wa video za mizaha ya kisiasa amekana madai hayo akisema hayana msingi wowote.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katika kipindi cha miaka michache iliyopita mamia ya watu wamekamatwa nchini humo baada ya kutoa matamshi ya kumsema vibaya rais Mugabe na kushtakiwa chini ya sheria iliyopitishwa majuzi inayochukulia swala la kumkosoa rais kuwa kitendo cha kihalifu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ni hivi majuzi tu ambapo rais Mugabe alimteua waziri ambaye kazi yake inahusika tu na usalama na udhibiti wa kilicho mitandaoni kinachoihusu Zimbabwe.

Asili:BBC

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.