kwamamaza 7

Zimbabwe kushuhudia demokrasia mpya-Rais mtarajiwa Emmerson Mnangagwa

0

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema nchi yake  inashuhudia mwanzo wa demokrasia mpya.

Mnangagwa, ambaye anatarajia kuapishwa kushika wadhfa wa Urais wa nchi hiyo siku ya Ijumaa, amesema kipaumbele chake ni kujenga upya uchumi wa nchi hiyo na kuunda ajira mpya kwa idadi kubwa ya watu wasio na ajira.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Katika hotuba yake hiyo, aliyokolezwa na maneno yaliyokuwa yakitumika wakati wa vita vya uhuru wa nchi hiyo, Bwana Mnangagwa alilishukuru jeshi la nchi hiyo, ambalo liliingilia kati baada ya yeye kufukuzwa na Rais Robert Mugabe na kuweza kufanikisha hali iliyopo sasa kwa amani.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Makamu huyo wa Rais wa zamani anayesubiri kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo alirejea nchini Zimbabwe mapema jana.

Aidha alifahamisha kuwa aliikimbia nchi hiyo baada ya kutishiwa maisha yake baada ya kufukuzwa katika nafasi yake hiyo.

Asili:BBC

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.