kwamamaza 7

Zambia: Mahakama yapinga kuwafukuza Wanyarwanda wawili walioshtakiwa kuwa wapelelezi wa Rwanda

0

Mahakama  Kuu nchini Zambia imepiga marufuku uamuzi wa Waziri wa Mambo ya ndani kuwafukuza Wanyarwanda Innocent Habumugisha na Egide Rwasibo ambao mwaka 2015 walishatkiwa  kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Mahakama imesema jambo hili halikufuata sheria kwani lilitekelezwa kisiri.

Pia wanasheria wa washtakiwa wameeleza waziwazi wateja wao wangelipata matatizo  kurudishwa nchini Rwanda kwa kuwa walikaribishwa nchini Zambia kama wakimbizi.

Kwa sasa, Habumugisha ambaye ni daktari na mwenzake Rwasibo ambaye ni mwanafunzi katika chuo Kikuu wangali nchini Rwanda kwa mujibu wa  The EastAfrican.

Habumugisha alisema kwamba nchini Zambia kuna Wanyarwanda wenye msimamao mkali ambao huwashtaka wapinzani wao kuwa wapelelezi wa Rwanda kwa kuwafukuza nchini.

Ikumbukwe kwamba kuna idadi kubwa ya Wanyarwanda nchini Zambia ambao wengi huwa kwenye shughuli zao za kibiashara.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.