kwamamaza 7

Zaidi ya 20 wameuawa katika mapambano ya makundi yenye silaha

0

Watu zaidi ya 20, wakaaji wakiwa wengi waliuawa katika mapambano kati ya makundi yenye silaha sehemu iitwao Bakouma nchini Centrafrika wiki hii.

Mapambano hayo yalikuwa kati ya wale waliokuwa wapiganaji wa Anti Balaka na Seleka, na yalianzia katika vijiji karibu ya mji wa Bakouma kama vile husema AFP.

Wengi waliofariki ni raia ila hesabu yaweza ongezeka kwa sababu hadi sasa mapigano huendelea.

Msemaji wa jeshi la umoja wa mataifa kwa kuzingatia amani huko Centrafrika, Vladimir Monteiro, alisema ya kwamba walikosa jinsi ya kwenda huko kwa sababu wapiganaji walibomoa kilala.

Sehemu hio hujulikana kuwa na mali asili ya Uranium, iliyo uzwa na kampuni ya Ufaransa “Areva” wakati wa utawala wa Francois Bozize ila walisimamisha huduma za uchimbaji mwaka wa 2012.

Mabishano Centrafrika yalitokana na waumini wa Seleka kutoka Islam na Anti Balaka wa Kikristu, hata kama pande zote mbili walitia saini kwa mkataba wa amani wakiwa Brazzaville, ila sasa mapigano ni sehemu tofauti za nchi.

Mwanzo wa mwaka huu walihesabu watu 400.000 waliohamishwa na mapigano.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.