kwamamaza 7

Weasel ambisha matusi baba yake juu ya mali ya Goodlyfe

0

Douglas Mayanja maarufu kama Weasel amembisha matusi baba yake Gerald Mayanja baada ya kutoa maoni husika na usimamizi wa mali miliki ya kundi la bin yake na marehemu Mowzey Radio.

Bw Gerald Mayanja amependekeza kuwa wangeliuza mali kisha kila mmoja  akapata gawo lake. Baada ya kusikia hili,Weasel amemuambia baba yake kuwa ni mjinga na maneno mengine ambayo Bukkede imeeleza kuwa siyo vizuri kupitisha mdomoni.

Weasel amesema”oli musilu(…)”yaani wewe ni mjinga.Hata hivyo, mzazi wake kupitia simu amesema kwamba mambo haya amemuachia Weasel mwenyewe kujadiliana.

“Sina  uhusiano na mambo yale,niliwaacha kuyatatua wenyewe” Gerald Mayanja ametangaza.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“Nami pia sina baba yangu,aliaga dunia lakini masuala yangu najitatulia mwenyewe,hana budi kutatua yake kwani yeye ni mtu mzima zaidi ya miaka 18”Mzazi Gerald ameongeza.

Pengine mzee Gerald amesema kuwa hawezi kufanya lolote kama hawataki kumsikiliza.

Pamoja na haya,mwanasheria wa marehemu Mowzey Radio,John Katende amewaita wanafamilia husika ili kutaja mali alizoziacha marehemu na kufanya mahojiano.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.