kwamamaza 7

Waziri wa sheria awazuru watoto waliotoka barabarani

0

Waziri wa sheria wa Rwanda Johnston Busingye pamoja na viongozi wengine wamewazuru watoto wanaopatiwa elimu katika Kinigi Transit Center katika wilaya ya Musanze, mkoa wa kaskazini. Waziri Busingye aliwatembelea leo asubuhi 18 Oktoba 2016.

Aliwaambia watoto hawa waliotoka barabarani na kutumia dawa za kulevya na tabia nyingine mbaya mithili ya umalaya, kwamba ndio matumaini ya nchi.

“Namna mnavyotuona kama viongozi, tunazeeka pole pole. Warithi wetu hawatatoka gerezani, katika utumiaji wa dawa za kulevya; katika uwizi… bali watatoka kati yenu mliobadilishiwa maisha na kupewa elimu ya kutosha”.

[ad id=”72″]

Waziri Busingye aliwakumbusha kwamba sababu ya viongozi kuwazuru ni kuwakumbusha majukumu yao kama viongozi wa kesho. “Viongozi sote huwatembelea kwa sababu mko wenye thamani kwa nchi yetu ya Rwanda”.

Miongoni mwa watoto hawa walitoa ushahidi kuhusu faida hupata baada ya serikali ya Rwanda kuwakomboa kutoka katika uchafu wa uwizi, kutumia dawa za kulevya, kuzurura; nkd.

Kituo cha Kinigi transit center hupokea vijana kati ya 18 na 35 wakati wanapokosa nidhamu na kujiingiza katika shughuli za uzururuzaji, matumizi ya dawa za kulevya na mengine mabaya.

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.