kwamamaza 7

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda ajadiliana na Rais Kagame

0

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda,Sam Kutesa jana amemkuta na kujadiliana na Rais wa Rwanda,Paul Kagame ikuluni,Village Urugwiro mjini Kigali.

Taarifa za Chimpreports zinasema kwamba mkutano huu unalenga kutatua na kuongeza nguvu za ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda.

Taarifa hizi zinasimulia kwamba Rais Kagame amekuwa na “utulivu” kwenye mkutano huu uliohudhuriwa na waziri mmoja tu kwa upande wa Rwanda,waziri wa mambo ya nje wa Rwanda,Louise Mushikiwabo.

Inafikiriwa kuwa Waziri Kutesa amekuja kuhakikisha kwamba Uganda haina dhamira mbaya kwa Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ziara ya Waziri Kutesa nchini Rwanda imetokea baada ya jana serikali ya Uganda kujibu Rwanda kuhusu suala la Wanyarwanda waliokamatwa nchini Uganda.

Ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda ulianza kuenda miezi michache iliyopita juu ya kuwateka nyara wakimbizi,upelelezi,kutotimiza ahadi za miradi ya kiuchumi na mengine.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na Twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.