kwamamaza 7

Waziri wa maliasili ahudhuria mashindano ya kampeni za usafi

0

Sekta ya Remera wilayani Gasabo imeongoza miongoni mwa sekta 34 zinazounda mji wa Kigali katika mashindano yalipatikana jana 24 Disemba 2015 ya kumaliza miezi sita ya kampeni za kutoa elimu kuhusu usafi na usalama.

Mashindano kati ya Gasabo, Nyarugenge na Kicukiro yaani wilaya za mji wa Kigali; yalifanyikia kwenye uwanja wa Kigali Nyamiramo kwa ushirikiano wa polisi ya Rwanda na mji wa Kigali.

Wakati wa mashindano, Waziri wa maliasili Dkt Vincent Biruta alisifu ushirikiano wa raia wa Rwanda na shirika mbali mbali ili kukuza mabadiliko ya nchi kwa njia ya uongozi sahihi.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

“Rwanda hasa hasa Kigali, inajurikana kwa usafi; utamaduni ambao ungeendelea miongoni mwa wanyarwanda wote ili kupambana na shughuli za uhalibifu wa mazingira kama kutumia mifuko ya plastiki na kurusha uchafu majini kwani husababisha ugonjwa mbali mbali.”

Vincent Biruta Bwiza.com
Meya wa mji wa Kigali, Monique Mukaruriza; waziri wa maliasili Dkt Vincent Biruta (kati) na kiongozi wa polisi IGP Emmanuel Gasana

Meya wa mji wa Kigali  Monique Mukaruriza alisema katika tukio hilo kwamba kampeni zitaendelea na matatizo mengine ambayo hujitokeza mjini. “Tumemaliza kampeni hii…tumeanza sura mpya dhidi ya dawa za kulevya, mifuko ya plastiki, ukatili na unyanyasaji wa kijinsia;” Mukaruriza aliongeza .

Sekta ya Remera kutoka wilaya ya Gasabo ilipokea nyara na gari. Ilifuatiwa na Gisozi kutoka Gasabo ambayo alipokea tuzo ya kifedha ya milioni Rwf 2 na sekta ya Kimisagara kutoka Nyarugenge ilipewa milioni 1ya pesa ya Rwanda.

Kwa upande wa usafi, mashindano yalihusika na usafi wa mazingira na usafi wa maeneo ya umma pamoja na kuepukana na matumizi ya mifuko ya plastiki.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.