Home SIASA Waziri mkuu yakiri kuweko kwa pengo kati ya viongozi wa kike kwenye michezo ya Rwanda
SIASA - August 10, 2017

Waziri mkuu yakiri kuweko kwa pengo kati ya viongozi wa kike kwenye michezo ya Rwanda

Waziri mkuu wa Rwanda amesema hivi alipokuwa akiongoza mkutano wa viongozi wa wanawake wanaoshiriki kwenye uongozi wa ngazi za michezo. Mkutano huu ulikuwa na madhumuni ya kuwahimiza wanawake kushiriki kwenye ngazi za michezo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Waziri Anastase Murekezi anakiri kwamba licha ya kuweko kwa idadi kubwa ya wanawake kwenye ngazi za uongozi wa serikali kungali na pengo kubwa kwenye ngazi za uongozi za michezo.

“Wanawake na wanaume wako sawa kiuwezo na wana thamani sawa na kwa hivyo wanapaswa kuwa na fursa sawa”

Waziri Murekezi aliongeza kwamba Rwanda iliwapea nafasi ya mbele wanawake na kwa hivyo wanawake na kwa hivyo pengo liloko kati yao na wanaume linapaswa kuzibiwa na wakawa na fursa sawa.

Wanawake walioko kwenye uongozi wa michezo ni pamoja na asilimia 42.8 kwenye olympique na 16% kwenye shirikisho nyingine za michezo.

Viongozi wengine walisifu hatua ya Rwanda ya kuwaachia nafasi stahiki wanawake katika uongozi wan chi na wakapendekeza hali kuwa kama hivyo kwenye ngazi za michezo.

Izeduwa Derex-Briggs Kiongozi wa wa idara ya Umoja wa Kimataifa ya  wanawake katika Afrika ya Mashariki na kusini amesema “Rwanda ni mojawapo ya nchi yenye mfano mzuri wa kuigwa kuhusu uimarishaji wa usawa wajinsia”

Aliweka wazi kwamba mfumo wa ulipaji wa mshahara sawa unawezekana.

Viongozi wengine akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki nchini Burundi walisisitiza kwamba wanawake wanastahili nafasi kwenye ngazi za ungozi za michezo.

Kikao hiki ambacho kinafanyika kwa kipindi cha siku tatu kilianza kwa kuizuru Kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Kigali kwa waliohudhuria.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.