kwamamaza 7

Waziri mkuu Murekezi amepiga marufuku ibada maofisini

0

Waziri mkuu Anastase Murekezi amepiga marufuku ibada zinazofanyinya maofisini katika ngazi ya utumishi wa ngazi za umma ambazo zinatajwa kuzorotesha utendaji kazi na kusababisha kuwepo utoaji mbovu wa huduma.

Janvier Ndayizeye ambaye ni afisa habari katika ofisi ya waziri mkuu alisema marufuku hii ni kufuatia badhi ya watumishi wa umma kuyageuza maofisi kuwa nyumba za ibada, ambapo raia wakija kuomba huduma wanakosa mtu wa kuwahudumiya kama vile husema mtandao wa izubarirashe.

Wafanya ibada wengi hufanya hivyo katika wakati wa mapumuziko ambapo mapumuziko hao ni kuanzia saa sita hadi saa saba kwa mujibu wa sheria, ila kuna wengine saa saba ikitimia wanaendelea na ibada badala ya kufanya kazi.

Waziri mkuu Anastaze Murekezi amewaambia mawaziri wote kulivalia njuga swala hilo na kuhakikisha hakuna ibada zingine zinafanyika katika mazingira ya kazi.

Wale ambao wanahitaji kufanya ibada mapumuzikoni wameshauriwa kutafuta sehemu ambapo zipo kwa ajili ya ibada kama makanisa bila kujifungia maofisini.

Wanaopendelea bwiza.com iwatembelee na kuwatangazia habari kwenye bidhaa vyao wanaweza kutumia ujumbe kwenye barua pepe ya meckypro@gmail.com, ama wapigie simu kwenye nambari ifuatayo: 0784685981.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.