kwamamaza 7

Waziri mkuu awatolea wito majiji wa kijeshi kutenda haki

0

Waziri mkuu wa Rwanda Anastase Murekezi amewahimiza mahakimu wakijeshi waliokura kiapo kuwa waadilifu katika kazi yao, kwa kutowa haki sawa.

Amesema hivi alipokuwa akipokea viapo vya Lt. Col Déo Rusizana ambaye ni makamu Mwenyekiti wa Mahakama ya Kijeshi, na Cpt. Gerald Ntaganira, ambaye ni Jaji katika Mahakama ya kijeshi ambako aliwahimiza kukata kesi kwa weledi na uadilifu ambapo maamzi atamridhisha hata mwenye kupoteza kesi.

Akigusia maadili ya majaji, Waziri alisema

“Mnapaswa kuwa na nidhamu katika mambo yote mnayoyafanya na kila popote mlipo, jaji mwema zaidi ya kuwa mjeshi wa RDF wanaosifiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, anapaswa kuwa mfano kwa wengine, kuwa makini na mtenda haki kwa hivyo ndio itakayowafanya kutowatia hatia wenye kutokuwa nayo na kuwaona na hatia wenye kuwa nayo”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Lt. Col Déo Rusizana, makamu Mwenyekiti wa mahakama ya Kijeshi na Cpt. Gerald Ntaganira ambao wamekula kiapo walikuwa wameteuliwa na Mkutano wa mawaziri wa 26/05/2017.

Na hapo 28 Machi 2017 waziri mkuu alipokea vile vile viapo vya majaji wa mahakama ya Kijeshi watatu ambao ni Capt. Vincent NDAYISABA, Capt Christian KAYITARE na hata Lt. Claudine MUHAWENIMANA.

Hapo mwaka wa 2014, napo waziri mkuu alivipokea viapo vya Majaji na waendesha mashtaka wa Mahakama ya Kijeshi akiwemo rais wa Mahakama ya Kijeshi Brig Gen Andrew Kagame, majaji wenye daraja la kapiteni(Capt.) ambao ni Onesphore Rutagengwa, Samuel Kazenga, Jean Pierre Mutezintare na 2nd Lt. Annonciate Nyirabahorana wakati huu aliwahimiza pia kufanya kazi yao kwa weledi na uadilifu kwa kutekeleza kazi yao vizuri. Amewatolea wito hasa wa kutia nguvu katika kujadili kesi za watu wanaotaka kuvunja usalama.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.