kwamamaza 7

Waziri mkuu aomba raia kukuza ajira binafsi

0

Waziri mkuu wa Rwanda Dkt Anastase Murekezi amewambia raia kukuza kazi za kibinafsi badala ya kungoja ajira kutoka serikalini. Mwito umetolewa leo 18 Novemba 2018 wakati wa kuwapongeza washiriki wa masomo kuhusu mswada wa serikali wa ukuzaji wa ajira binafsi (NEP/KoraWigire).

Murekezi amewasihi raia kutia bidii katika kazi za kibinafsi pamoja na kazi za kiufundi ili kuepukana na ukosefu wa ajira.

Utafiti ulionyesha kwamba katika idadi ya wanyarwanda 5,590,000 wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi isipokuwa wanafunzi; serikali inakuwa na uwezo wa kutoa ajira kwa kiwango cha 3% na wengine 97% hulazimishwa kujitafutia kwenye sekta na ajira za kibinafsi.

Waziri mkuu Dkt Anastase Murekezi akionyeshwa jibini
Waziri mkuu Dkt Anastase Murekezi akionyeshwa jibini

Shirika za wilaya zimeamrishwa kujenga mahari pa kufanyia kazi za kibiashara na za kifundi panapojurikana kwa kienyeji kama ‘Agakiriro’; na hivi vijana kupata mavuno kwa majengo haya.

[ad id=”72″]

“Muanzie kwenye uwekezaji mdogo kisha mtapanua kimaendeleo. Muelekee kwenye majengo kufanyia kazi za kibiashara na za kifundi ili kukuza kazi za kiufundi na ajira binafsi. Wilaya ambazo hazijajenga mahali hapo, wanalazimishwa kufanya haraka na waliokamilisha kujenga kwenye cheo cha wilaya wanaweza kuendelea kwenye cheo cha kata,” Waziri alisema.

Mswada wa serikali wa NEP/KoraWigire ambao huhusika na uhamasishaji kuhusu ajira binafsi na kazi za kiufundi, umeanzishwa mnamo 2014 na wafadhiliwa 80,672 wamenufaishwa na mswada huu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.