kwamamaza 7

Wawili walio kata DASSO kwa upanga waliuawa kwa lisasi

0

DASSO (District Administration Security Support Organ), ni ngazi ya usalama ilio chukuwa nafasi ya “Local Defence”.  Ngazi hio ilianza kazi yao wakiwa na nguvu katika majukumu yao ila walikuwa wakipambana na wakaaji. Hadi sasa wawili ambao waliokata DASSO kwa upanga walifyetuliwa lisassi wakafa.

Tarehe 14 April ndipo Mbyariyehe Olivier, mwenyeji wa tarafa ya Rongi katika wilaya ya Muhanga, alikata DASSO wakati walimukuta akichoma makala katika ardhi ya serikali ya Ndiza na alipelekwa kwenye stesheni ya polisi ya Kiyumba.

Mbyariyehe aliye kata DASSO ni memba wa kundi ya vijana wanao julikana kama waharibifu ”Ibihazi”, wakihusika na kujigenga na maharibifu mengine.

Baada ya siku tatu, Mbyariyehe Olivier, akiwa kwenye stesheni ya polisi ya Kiyumba alijaribi kutoroka ila hakufanikiwa kwa sababu alipigwa lisasi na askarili polisi aliye kuwa kwenye ulinzi.

Taarifa hio imehakikishwa na aliyekuwa msemaji wa polisi ya Rwanda, ACP Celestin Twahirwa, akisema Mbyariyehe alipigwa lisasi akijaribu kutoroka, ilikuwa jumapili tarehe 16 April 2017 na akafariki, DASSO akiyekatwa ajulikana kwa jina la Hategekimana Jeremie alipata matibabu katika Hospitali ya Kabgayi ila tayari amekwisha toka hosptalini.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa hii hufanywa baada ya siku moja kijana mwengine allikuwa akifungiwa katika wilaya ya Rusizi, jimbo la Mangaribi, stesheni ya Kamembe akipigwa lisasi na kufariki, akijulikana kwa jina la Namahoro Jean Bosco naye alikuwa akishutumiwa kukata DASSO kwa upanga

Tarehe 20 April ndipo taarifa kasema kuwa Jean Bosco amepigwa lisasi kwenye stesheni ya polisi na polisi ya nchi kahakikisha kuwa taarifa hio ni ukweli kwa sababu alikuwa akitoroka.

Msemaji wa polisi ya Rwanda, ACP Theos Badege, alitangaza ya kuwa askali polisi mwenye alikuwa kwenye ulinzi hakuwa na namna nyingi isipo kuwa kufyetua lisasi.

DASSO ni ngazi ya usalama ambayo huaminiwa na raia 86.1% , polisi ikiwa 97.1% , ila jeshi la Rwanda wao ni 99.0% kama vile huonyesha utafiti uliofanywa na kituo cha nchi kinacho husika na uongozi RGB 2016.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Leki/bwiza

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.