kwamamaza 7

Watu zaidi ya 24 wafarikia katika tetemeko kubwa indonesia

0

Tetemeko kubwa la ardhi limeua watu zaidi ya 24 na kusababisha uharibifu mkubwa katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia. Maafisa wanasema watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyoporomoka.

Tetemeko hilo la nguvu ya 6.4 kwenye vipimo vya Richter lilitokea karibu na mji wa Sigli katika kisiwa cha Sumatra ambapo majumba mengi yameporomoka.

Shirika la utabiri wa hali ya hewa la Indonesia limesema hakuna hatari ya kutokea kwa kimbunga.

_92861770_4427f178-d55b-481b-868a-d0a23dba17a9
Majumba mengi yaporomoka hivi watu wengi wafarikia ndani

Taasisi ya Jiolojia ya Marekani imesema tetemeko hilo lilitokea karibu na pwani mwendo wa saa 11:03 asubuhi saa za huko (22:03 GMT Jumanne) katika kina cha 17.2km (maili 11) chini ya ardhi.

Said Mulyadi, naibu mkuu wa wilaya ya Pidie Jaya, eneo lililoathiriwa pakubwa na tetemeko hilo, ameambia idhaa ya BBC ya Indonesia kwamba huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

Mwaka 2004, mkoa wa Aceh uliathiriwa sana na kimbunga kilichosababishwa na tetemeko kubwa baharini. Watu 120,000 waliuawa mkoani humo.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.