kwamamaza 7

Watu wawili kutoka wilaya tofauti wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuwaua wake wao

0

Watu wanaowaua wanandoa wao wanaendelea kuzikabili adhabu kali, hii itakuwa onyo kwa wengine kama ilivyokuwa, jumatano hii kwa wanaume wawili waliohukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia wa kuwaua wake wao.

Tarehe 21 Juni mwaka 2017, Mahakama kuu ya Rusizi imemhukumu kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia kumuua mke wake.

Uhalifu huu ulitokea jioni ya tarehe 03 Mei 2017 karibu saa saba za usiku katika Kijiji cha Gasharu Sehemu ya Impala, tarafa ya Bushenge wilaya ya Nyamasheke.

Hii ilitokea mwanaume huyu alipotoka kuiba miwa kwa shamba la jirani na mke wake akamkatalia kuingiza miwa hiyo ndani ya nyumba alikuwa amemwacha akilala kitanda usikuu huo.

Mwanaume huu alitumia nguvu kuingiza miwa hiyo na alipoingia alichukua mti mpana wa kusaga na kumpiga kichwani mara mbili na akapoteza fahamu. Watoto waliita jirani kwa msaada na wakampeleka hospitali ila tu imekuwa sio mapema kwa kuwa alifariki mara tu baada ya kufikishwa hospitali.

Ingawa mhalifu huu Ntagozera Stanislas alikiri hatia na kuomba msamaha, mahakama haikulitilia maanani kwa sababu alimuua kikatili.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kesi nyingine kuhusu mauaji ilisikizwa wilayani Gicumbi, ambapo tarehe 21 Juni mahakama ilisoma maamuzi ya kesi ambapo Rutembeza Vincent alikuwa akishtakiwa kumuua mke wake Kubwimana Beatha kutoka tarafa ya Giti, sehemu ya Murehe kijiji cha Gatare

Baada ya mahakama kumtia hatia, alihukumiwa kifungo cha maisha jela kama ilivyopendekezwa na uendeshaji mashtaka katika usikizaji kesi wa hadharani kwenye eneo ambalo uhalifu ulitokea tarehe 01 Juni 2017.

Ingawa mshitakiwa alikiri hatia kwa kusema kwamba alimchunga alipokuwa akisinzia na kumkatakata kwa kutumia panga na kusema kufanya hayo kulitokana na kuwa mke huyo hakumwacha kuuza mali.

Mahakama ilimhukumia kulingana na masharti ya ibara 142 ya kitabu cha kanunu za adhabu ambayo inaeleza kwamba anayepatikana na kosa la kumuua mwanandoa wake anaikabili hukumu ya kifungo cha maisha jela

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.