kwamamaza 7

Watu watatu wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuuza Bangi

0

Jeshi la Polisi linawashikilia wakazi watatu wa Talafa ya Kimisagara kiini cha Kamuhoza Wilaya ya Nyarugenge,  kwa tuhuma za kuuza bangi ambapo wamekutwa wakiwa na kilo 450 za bangi nyumabani kwao .

Bangi hizo zimekutwa zikiwa zimefungwa katika vifurushi 100  ambapo kila kifurushi kirikuwa kinauzwa kati ya faranga 150 na 200 wakati kuna bangi nyingine ambayo irikuwa imefungwa katika mifuko mikubwa.

Walio kamatwa kwa tuhuma za kuuza bangi ni pamoja na  bwana ambae alikuwa mlinda geti ambapo kazi yake ilikuwa  ni kufuatilia jinsi gani bangi hiyo inavyo ingizwa hapo nyumbani, mwingine  ni  bwana mwenye mji ambae ndie aliye kuwa akihifazi bangi hizo na kuzitafutia wateja.

Wakati mwingine aliye kamatwa ni muendesha Daradara ambae shughuli zake zilikuwa ni kuleta bangi hizo kwenye pikipiki na kuzifikisha hapo nyumbani.

Wakati  Polisi ilipo kuwa ikiwaonyesha wanahabali  washukiwa hao, wawili wamekana tuhuma hizo wakisema kuwa walikuwa hawajuwi nini kirichomo ndani ya mifuko hiyo, lakini muendesha daradara yeye amekili akisema kuwa anaomba ladhi  hatarudia tena kufanya shughuli hizo za kuuza bangi.

Mwendasha daradara huyo amesema kuwa yeye amefanya kinyume na kazi zake, kwani yeye kazi yake ni kupeleka abilia sio kubebe mizigo, pia amekili kwamba yeye  amefanya hivyo  kwaminajili ya kujipatia tija.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Msemaji wa jeshi la  Polisi nchini ACP Theos Badege amesema kuwa  chanzo cha ku kamatwa kwa washukiwa hao nikutokana na talifa ambazo zilikuwa zimetolewa na wana kijiji hao.

Msemaji wa Polisi amesema kuwa Polisi  imelivalia juga swala la wanao uza bangi, Pia amewahamasisha  vijana chipukizi kuepukana na tabia hiyo mbaya ya kuuza bangi na kusema kuwa kuna shughuli zingine ambazo wanaweza wa kafanya pasipo  kuuza hayo madawa ya kulevya.

Watuhumiwa hao watakapo patikana na hatia ya kuuza bangi, wataazibiwa chini ya shelia  kifungu  594 katika kitabu cha shelia,  amabapo  kifungo hicho kinasema kwamba kila mtu anae patikana na tuhuma za kuuza bangu au madawa yakulevya kwa ujumla, hupewa kifungo jera cha mwaka mu moja hadi miaka mitatu. na  faini ya faranga elfu hamsini hadi laki tano kwa mjibu washelia.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

John Bagabo@Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.