kwamamaza 7

Watu 35 wauawa wakati wa makesha wa mwaka mpya wa 2017

0

[ad id=”72″]

Kiasi cha watu 35 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanyika wakati wa mkesha wa Mwaka Mpya kwenye kilabu moja ya usiku katika mji mkuu wa Uturuki, Istanbul.

Gavana wa jimbo hilo, Vasip Sahin, amesema anayachukulia mashambulizi hayo, ambayo pia yamewajeruhi watu 40, kuwa ya kigaidi.

Gavana huyo amesema mshambuliaji aliingia kwa nguvu katika kilabu hiyo ya usiku iitwayo Reina, baada ya kuwafyatulilia risasi na kuwaua afisa wa polisi pamoja na raia mmoja waliokuwa mlangoni.

Watu kati ya 700 na 800 wanakisiwa kuwapo ndani ya kilabu hiyo ya usiku, wakati ilipovamiwa. Picha za televisheni za shirika la habari la CNN zilionesha magari ya kubeba wagonjwa pamoja na magari ya polisi yakiwa nje ya kilabu hiyo.

Usalama umeimarishwa mjini Istanbul, huku ikiripotiwa polisi 17,000 kufanya doria katika kipindi hiki cha sherehe za Mwaka Mpya ikiwa ni tahadhari kutokana na hofu kuwa mji huo unaweza kulengwa na mashambulizi ya kigaidi.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.