kwamamaza 7

Watu 2 wako mbaroni wakishutumiwa kuiba waya za umeme

0

Polisi ya Rwanda katika wilaya ya Kirehe wamekamata watu wawili wakishutumiwa kuiba waya za umeme za kampuni inayohusika na nguvu za umeme (Energy Utility Corporation Limited – EUCL), zenye urefu wa meta 20.

Wanaofikiliwa kufanya hayo ni Ukozivuze Ezechiel, mwenye umri wa miaka 65, na jirani yake  Rutayisire Robert mwenye umri wa miaka 35.

Walikamatwa tarehe 22 Januari asubui mapema baada ya kuzishusha hapo katika kiini ya Nyamugari, kata ya Nyamugari anapoishi Ukozivuze Ezechiel. Hao wote wawili wapo kwenye stesheni ya Nyamugari, upelelezi ukiendelea.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Msemaji wa polisi ya Rwanda katika jimbo la Mashariki Inspector of Police (IP) Emmanuel Kayigi, amesema ya kuwa kuiba vifaa vya umeme na mengine ya msingi ni kuharibu maendeleo ya nchi kwa ujumla, kwa hio ni uwajibu kwa kila mtu kujua usamini wa hayo na kuyazingatia, na kushotea kidole yeyote anayejaribu kuharibu.

IP Kayigi amewashukuru walio toa taarifa ambayo ilisukuma kukamatwa kwa watu hao wawili wakiwa na waya za umeme, na kujilinda makosa yoyote.

Katika kitabu cha sheria ya Rwanda, makala 406, husema ya kuwa anaye fanya makosa kama hayo na mengine ya uhusiano, ataazibiwa kufungwa kati ya miaka miwili hadi tano na kutoa garama ya pesa mara 10 ya yale aliyo haribu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google”]

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.