Home MICHEZO Watoto 80 wafundishwa sheria na kanuni za mchezo wa Wavu (Volleyball)
MICHEZO - December 27, 2016

Watoto 80 wafundishwa sheria na kanuni za mchezo wa Wavu (Volleyball)

[ad id=”72″]

Shirika la mchezo wa  Volleyball nchini Rwanda (FRVB) limewafundisha watoto ambao wana umri wa miaka chini ya 14 kanuni na sheria za mchezo wa Volley Ball kwenye kikao cha shule “Groupe Scolaire de Karubanda”.

Katibu wa shirika hilo FRVB, Hatumimana Christian ametoa  taarifa na kusema kwamba watoto hao wamefanya muda wa wiki moja wakifundishwa pia namna gani kucheza mchezo wa Volley Ball pia na kufahamu sheria na maelekezo ya mchezo huo.

Hatumimana amesema eti “ mafundisho ya watoto hawa ni wale ambao walikua na umri chini ya miaka 14, baada ya hapo tunajiandaa kuwafundisha pia wenye umri usio zidi miaka 17 January mwaka wa 2017 “, na amesema pia watoto wenye wamepata mafunzo  ni 80, pakiwemo wavulana 40 na wasichana 40.

Walitarajia msaada kutoka uwaziri wa michezo(MINISPOC)  ipatayo miliyoni 16, ila wakapewa miliyoni 8 pekee, na mafunzo ya kituo cha kwanza walitumia pesa miliyoni inne na wanaamini kituo chengine watatumia miliyoni inne pia.

Kituo cha kufuata kitafanyika katika jimbo la mashariki, wilaya ya Rwamagana kwenye kikao cha shule “St Aloys”.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[ad id=”72″]

Leki@bwiza.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.