kwamamaza 7

Watatu wauawa karibu na mpaka wa Rwanda na Burundi

0

Watu watatu wakiwemo mwanamke Esperance, mtoto wake wa miaka 13 na mwingine wa mwaka mmoja na nusu wamefariki katika mashambulizi  jumapili karibu na mpaka wa Rwanda na Burundi mkoa wa Cibitoke.

Kwa mujibu wa taarifa za Ikiriho hawa waliuliwa na watu wenye silaha  kutoka upande wa Rwanda na kushambulia familia ya Ernest Ndayisenga.

Hawa walitoka upande wa Rwanda majira ya usiku wa manane kutoka mto wa Ruhwa baada ya jeshi na walinzi wa usiku kuondoka katika hilo eneo.

Hili ni baada ya wakazi wa hili eneo wiki iliyopita kukimbia kisigino kisogoni kwa kusema kuna watu kutoka Rwanda wanaotaka kuwaua.

Hata hivyo, hizi taarifa zilikuwa ni fununu tu kama ilivyohakikishwa na uongozi wa ndani nchini Burundi.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.