kwamamaza 7

Watakaopigania tuzo ya mwanasoka bora zaidi Afrika 2016

0

Wachezaji watano watakaoshindania Tuzo  ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016 wametangazwa.

Wachezaji hao ni Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane na Yaya Toure.

Wachezaji hao watano walitangazwa wakati wa kipindi maalum cha moja kwa moja runingani Jumamosi.

Mshindi atachaguliwa na mashabiki wa soka ya Afrika kutoka kila kona ya dunia. Mashabiki wana hadi saa 18:00 GMT tarehe 28 Novemba kumpigia kura mchezaji wanayempenda.

Mnamo Jumatatu, 12 Desemba, mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa moja kwa moja kwenye runinga ya BBC Focus on Africa pamoja na redio, kuanzia saa 17:35.

Aubameyang ameorodheshwa kwa mwaka wanne mtawalia, mshindi wa mwaka 2011 pia ameorodheshwa kwa mwaka wa nne, Mahrez ndiye mchezaji pekee ambaye hajawahi kuorodheshwa kushindania, Mane alishindania mara ya kwanza mwaka jana naye mshindi mara mbili. Toure ameorodheshwa kwa mwaka wa nane mtawalia.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Aubameyang amekuwa na kipindi cha kufana sana mwaka 2016, amefunga mabao 26 (kufikia wakati wa kuandika makala hii) katika klabu yake ya Borussia Dortmund nchini Ujerumani

Alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika kutawazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Bundesliga, raia wa kwanza wa Gabon kushinda tuzo ya Shirikisho la Soka Afrika ya mchezaji bora wa mwaka Afrika, na ameorodheshwa miongoni mwa wachezaji wanaoshindania tuzo ya mchezaji bora duniani mwaka 2016, tuzo ya Ballon d’Or.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.