kwamamaza 7

Wanyarwanda wawili ‘watekwa nyara’ nchini Uganda

0

Wanyarwanda wawili Sendegeya Théogene na Magezi Emmanuel walitoweka mwaka uliopita  baada ya kukamatwa kwenye kituo cha jeshi mjini Mbarara.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini Rwanda wanafamiia wao wangali katika  hali ya wasiwasi ya maisha ya wanafamilia wao juu ya kutojua walipofungiwa.

Hayo ni baada ya visa kadhaa vya Wanyarwanda kukamatwa, kufungwa jelani kwa kushakiwa kuwa wapelelezi wa Rwanda.

Kuna tuhuma kwamba Sendegeya na Magezi walikamatwa na upelelezi wa  jeshi nchini Uganda (CMI) na kufungiwa katika majengo ya siri.

Haya ni baada ya serikali ya Rwanda kuwashauri wananchi kutokwenda nchini Uganda juu ya usalama wao.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.