kwamamaza 7

Wanyarwanda waonywa na Benki kuu kutoshiriki shughuli za D9 Club

0

Wanyarwanda wanaonywa kutoshawika na kushiriki D9 Club kwa kuwa vitendo vyake ni vya utapeli vinavyolenga kuwanyanganya watu fedha zao.

John Rwangombwa, Gavana wa Benki Kuu ya Rwanda, amesema kwamba shirika hilo halina ruhusa ya kuendesha shughuli zake na hutumia njia za mtandao zinazojulikana kama Pyramid Scheme kwa Kingereza. Mfumo huu ni wa uekezaji fedha ambapo watu huwekeza fedha na baadaye kutumika kama wakala na wakawaleta watu wengine ambao huwekeza fedha pia ambazo watapata malipo fulani na ikaendelea kiivyo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Benki kuu ya Rwanda imepiga marufuku shughuli za shirika hili ambalo lilieneza matawi kwenye nchi kama Kenya, Uganda na Zambia. Kwa mjibu wa tangazo la Benki kuu, shirika hili lilianza shughuli zake bila ruhusa kupitia hadhi ya Smart Protus Magara ambaye alikuwa na uadhifa wa matangazo katika nchi ya Uganda.

Kwa hiyi, Benki kuu ilipata fursa ya kuhimiza taasisi za fedha kuchukua hatua za kusitisha upelekaji pesa na shirika hili na kuzuia kusambaa kwake nchini kote.

Siku za hivi karibuni kulisitishwa shughuli za shirika kama hili lililokuwa linaitwa Tianshi na QuestNet baada ya kushindwa kuonyesha jinsi ya kulipa kodi

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.