kwamamaza 7

Wanyarwanda wanaoishi Uganda wako tayari kwa uchaguzi wa rais- Balozi Mugambage

0

Wakati shughuli za kampeni za mwisho mwisho kwa wagombea urais zinazidi kupamba moto hapa Rwanda, wanyarwanda wanaoishi nje ya nchi nao hawakuachwa nyuma ikiwa wanyarwanda wa nchini Uganda nao wanajitayarisha kupiga kura hapo Ijumaa tarehe 4.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kulingana na tarifa aliyoipa tovuti ya Igihe.com, balozi wa Rwanda nchi Uganda amesema kwamba yote yamekwisha andaliwa na wanyarwanda wapatao 7000 wako tayari kupiga kura.

“wanyarwanda wa hapa wako tayari, tuna takriban wanyarwanda 7000 waliojisajili kupiga . Kuna kituo kimoja cha kura ambacho kiko hapa kwenye balozi na wanyarwanda watakaotoka pande tofauti za nchi hiyi watabudi kufika hapa Kampala kwa ajili ya kura”. Asema Balozi Frank Mugambage

Balozi huyu aliendelea kusema kwamba kumekuwa na mikutano mingi ya kuwahamasisha wanyarwanda wanaoishi pande zote za Uganda kushiriki kura kwa wingi.

Licha ya kwamba kuna wagombea watatu wanaowania kiti cha urais wa Rwanda ambao ni mgombea huru Mpayimana Phillipe, Frank Habineza wa chama cha Green na hata Paul Kagame wa chama cha RPF, balozi Mugambage athibitisha kwamba Paul Kagame ndiye atakaye pata kura nyingi kulingana na idadi ya watu walioasilisha nyaraka zao wakiomba kura ya maoni ( referendum ) kufanyika ili Kagame aweze kuwania muhula mwingine.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“wakati wanyarwanda walipoasilisha nyaraka na wanyarwanda wa hapa walifanya hivyo hivyo na ikiwa mnakumbuka matokeo ya referendum yalikuwa 98.6% . kwa hivyo tu matokeo yanaeleweka”.

Isipokuwa wanyarwanda ambao watapigia kura nchi humo kuna wengi ambao wameanza safari za kurudi Rwanda ili waweze kupigia kura maeneo ambayo walijisajilia.

“wengi waliisha chukua mabasi wakija kupigia kura hapo Rwanda ambako walijisajilia”.

Nchi ya Uganda ni nchi jirani ambayo huenda ndio nchi ya kigeni inayokaliwa na wanyarwanda na hili hutokea na kutafuta kazi, biashara kati ya wananchi hizo mbili na hata historia ya ukumbizi kwa wanyarwanda hapo miaka iliyopita.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.