Mahakama kuu ya Jimbo la Kayanza yawahukumia wanyarwanda 8 baada ya kupatikana na kosa la Kuvuka mpaka kuingia Burundi bila Vitambulisho.

Wote wakiwa 8 walikamatwa katika kilima cha Ryamukoma, wilaya ya Kabarore, katika jimbo la Kayanza, wakijumuisha kwa wengine 12 ambao wanafungiwa katika Gereza ya Ngozi, ambao walikamatwa wakijaribu kusafirisha kahawa ya Burundi kuileta Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kuna habari nyingine zinazosema kwamba kuna gari lingine lililokamatwa kwenye mpaka wa Burundi na Tanzania, likibeba tani zipatazo 26 kuenda Tanzania. Munyarwanda dereva wa hili gari nae alihukumiwa kifungo cha miaka mitano, na gari kushikiliwa na Serikali ya Burundi.

Mahakama kuu ya Jimbo la Muyinga ambayo ilikata kesi hii, iliamuru pia kuwa maharagwe haya ambayo amekuwa akisafirishwa kwenda Tanzania atapewa wasiojiweza Burundi.

Wanyarwanda wanaendelea kukuta matatizo hapo Burundi, Na hii ni baada ya hizi nchi mbili kusitisha uhusiano wa Kidiplomasia mnamo miaka 2 iliyopita. Na ni wakati ampapo serikali ya Burundi inaishtumu ya Rwanda kuhusika na vitendo vya kuuvunja usalama nchini Burundi, madai ambayo serikali ya Rwanda inatupilia mbali.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.