kwamamaza 7

Wanyarwanda 3 wanaotuhumiwa uhalifu wa mauaji ya kimbari wasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu maombi yao

0

Tarehe ya 29 Juni 2017 ndipo wanyarwanda 3 watajua uamuzi wa mahakama ambapo uendeshaji mashtaka umewatakia kesi yao kuendeshwa na mahakama nyinginene isiyo ile inayoendesha kesi za uhalifu dhidi ya kibinadamu.

Mojawapo ya watuhumiwa ni Fabien Neretse ambaye anatuhumiwa kuunda kundi la waasi la interahamwe, kuandaa na kushiriki katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi na hata kuwazuia watu waliokuwa wanataka kukimbia mauaji hayo.

Kesi ilianzishwa na mke mbelegiji ambaye mumewe mnyarwanda aliuawa pamoja na bintiye na hata dadake tarehe 9 Aprili 1994.

Alitikamatwa nchini Ufaransa tarehe 29 Juni 2011 na kupelekwa ubelgiji baada ya miezi miwili na baadaye akawachiwa huru kwa muda.

Watuhumiwa wengine ni Emmanuel Nkunzuwimye na Ernest Gakwaya, waliokuwa washiriki wa makundi ya Interahamwe, wahalifu hawa wanashtakiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari na hata uhalifu wa kivita, wanatuhumiwa kushiriki katika mauaji kwenye uwanja wa Nyamirambo. Hawa walikamatwa Ubelgiji na kuachiliwa huru baadaye kwa muda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Uendeshaji mashtaka umewatakia kesi yao kupelekwa katika mahakama isiyo ile inayoendesha kesi za uhalifu dhidi ya kibinadamu kama uhalifu wa mauaji ya kimbari, mauaji na kadhalika.

Mahakama ya “tribunal correctionnel” nchini Ubelgiji ina mamlaka ya kutoa hukumu ya miaka kati ya 30 na 40, ila inaweza ikatoa pia hukumu kai kama zile zinazotolewa na mahakama ya Assises “cour d’assises” wakati kuna ushahidi wa kutosha.

Mpaka sasa Wanyarwanda wengine saba wamekwisha hukumiwa na mahakama za Ubelgiji kwa uhalifu wa mauaji ya Kimbari na walihukumiwa vifungo kati ya miaka 8 na 20.

Katika mahakama za correctionnel kesi huendeshwa na majiji wa kifundi na kuna imani kunatolewa haki.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.