Swahili
HABARI MPYA

Wanyarwanda 1,468 wakubaliwa kuhama nchini Zambia

Serikali ya Zambia jana kwenye kambi ya wakimbizi ya Meheba nchini Zambia imeamua kuwahamisha kwa mpito Wanyarwanda 1468 nchini  humo.

Waziri kwa masuala ya Wakimbizi nchini Zambia, Stephen Kampyongo  ametangaza hata kama kunahitajika ushirikiano na nchi nyingine,serikali yake imeamua kuwahamisha wakimbizi  hawa asili ya Rwanda.

Kiongozi kwa niaba ya UNHCR, Pierrine Aylara ameshukuru uamuzi wa kibinadamu wa Zambia hasa kwa Wanyarwanda walioamua kuishi nchini humo baada ya Rwanda kuondoa hali ya ukimbizi.

“Wakimbizi wanakaribishwa nchini Zambia bila tatizo.UNHCR inahamasisha  Zambia kuendelea kuwahamisha wakimbizi kwa kufuata misingi ya maendeleo ya nchi hii”

Aylara amesisitiza  UNHCR itaendelea kusaidia serikali ya Zambia kutoa suluhsho za masuala ya wakimbizi.

Zambia inahudhumia wakimbizi 74,000 na baadhi yao ni asili ya Rwanda wakiwemo 4,000 waliokimbia mwaka 1959 na 1998.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com