kwamamaza 7

Wanawake kutoka kijijini waeleza changamoto kadhaa zinazowazuia kupiga hatua ya maendeleo

0

Wanawake wanaoishi kijijini wanasema kwamba  siku hizi wana vipingamizi kadhalika vinavyowazuia kupiga hatua ya maendeleo kama vile kubaki nyumbani kila siku wakifanya kazi za ambazo hazilipiwi fedha.Jambo amabalo wanaeleza kuwa ndilo chanzo kwao kubaki nyuma katika maendeleo.

Akizungumza na Bwiza.com mmoja wao,Mujawamariya Berancille ambaye ni  anaishi kijijini Gifumba,tarafa ya Nyamabuye amesema kwamba isipokuwa yeye kwenda na kukaa nyumbani akifanya kazi za kawaida za huko,hana lolote lingine amabalo laweza kumsaidia na ye akapata namna ya kumiliki fedha mfukoni.Mujawamariya ameeleza kwamba kazi za nyumbani zinachukua muda mrefu wao kwa kuwa huwa ni nyingi sana kama kuchota maji,kutafuta kuni,kupika na mengineyo.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Amesema”Nikiamka asubuhi huenda kuchota maji nikiruudi huenda kutafuta kuni iliniweze kupika chakula badaye kutafuta nyasi za mifugo kasha nikaanza kupika na mengine ambayo yanahitajika kusafishwa nyumbani”.

Mujawamariya ameongeza kuwa anakosa wakati wa kupumzika kwa sababu ya kazi nyingi za kila siku na kujikuta yeye hawezi hata kutafuta kazi nyingine kwani mpanda farasi wawili hupasuka msamba.Ana sema kwamba  hili husababisha kutegemea mume wake ambaye  kazi yake ni kubeba mizigo kila wakati anapohitaji fedha.

Mzazi huyu amendelea kwa kusema kuwa maisha ya wanawake kutoka kijijini yanafanana.Ofisa wa shirika la Action Aid,Uwiragiye Anatole amesema kwamba kulingana na utafiti walioufanyia katika wilaya ya Nyanza,Nyaruguru,Gisagara,Karongi na Musanze waligundua kuwa mwanamke hutumia masaa saba akifanya kazi za nyumbani ambazo hazilipiwi.Ameongeza kwamba kazi za mwanamke kutoka kijijini zinatia maisha yake hatarini kama vile kunyanyaswa na ww miliki wa mashamba akitafuta kuni,kupigwa akichota maji n.k

Kiongozi huyu ameeleza kwamba suluhisho la kutatua tatizo hili ni  yeyote kupa uzito wa jambo hili hata ikiwa serikali,wanawume,asasi za kiraia.Amesema”Walioanzisha ule mkakati wa ‘nkunganire’ kwa wakulima,waweza kuanzisha ‘nkunganire’ ya kununua Gesi kwa kurahisisha kazi ya mwanamke ya kutafuta kuni.

Anatole amaeongeza kuwa kuiweka mipango kamili ya maendeleo kama vile kuleta maji karibu na vijiji kama m500,matumizi ya gesi yaweza kuboresha maisha na maendeleo ya mwanamke kutoka kijijini kwa kuwa watapata fursa ya kuhudhuria mipango ya serikali,kuhojiana na wenzao na kupata mawazo mpya ya kujiendeleza wenywe.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.