kwamamaza 7

Wanawake huhusika zaidi na biashara haramu ya kuvuka mipaka

0

Wanawake wa Rwanda wanasemekana kufanya biashara haramu ya kuvuka mipaka zaidi ya wanaume, kama hutangazwa na wizara ya viwanda, biashara na shughuli za shirika la Afrika la mashariki.

Mnamo mwaka wa 2015, kulikuwa na mali nyingi iliyouzwa nje kwa njia za panya inayostahili milioni 108,3 za dola ya Marekani na nyingine inayostahili milioni 22 za dola ya Marekani iliyoingizwa nchini Rwanda kiharamu.

Katika mkutano ulianzishwa jana nchini Rwanda ambao huhusika na kuepukana na biashara haramu zinazovuka mipaka, waziri wa viwanda, biashara na shughuli za shirika la Afrika la mashariki; Francois Kanimba alisema kwamba kwa ushirikiano na EIF (Enhanced Integrated Framework) iliyotaarisha mkutano huo, wataunga mkono kutafuta pamoja azimio la biashara haramu.

[ad id=”72″]

Waziri kanimba alisema, “EIF ni mmoja miongoni mwa wadau madhubuti wa maendeleo nchini Rwanda. Msada wa EIF utasaidia serikali ya Rwanda kukuza maendeleo na uchumi na kuwasaidia wananchi wenye kuwa na maisha magumu pamoja na wanawake ambao hufanya biashara haramu za kuvuka mipaka.”

Siku zilizopita, kuna wanawake wa mkoa wa kaskazini waliwekwa mbaroni wakishitakiwa kuwa na vinywaji haramu walinunua kwa wingi kutoka nchini Uganda.

Takwimu huonyesha kwamba kati ya 70 na 80% ya biashara inayovuka mipaka hufanywa na wanawake, na 90% miongoni mwao hufanya biashara haramu ambayo husababisha hasara kubwa kwa nchi na eneo kwa ujumla.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.