kwamamaza 7

Wanaume zaidi 150 watuhumiwa kupachika mimba wasichana Wilayani Kicukiro

0

Viongozi Wilayani Kicukiro wamewasilisha kwa Ofisi ya Upelelezi nchini (RIB) orodha ya wanaume 168 ambao wanaotuhumiwa kuwapachika mimba wasichana wenye umri wa miaka chini ya 18.

Viongozi wilayani humo wametangaza hawa wasichana walipachikwa mimba mwaka 2015-2019 na orodha hii iliundwa mwishoni mwa mwaka 2018.

Kiongozi wa Wilaya ya Kicukiro, Dk. Nyirahabimana Jeanne ameambia vyombo vya habari nchini kwamba wanapambana na hili suala na wameisha toa orodha ya wanaume wanaotuhumiwa vitendo vya kuwapachika mimba wasichana.

“ Orodha tuliyotunga, inaonyesha waschana 168 na majina ya wanaotuhumiwa kuwapachika mimba. Tuliwajulisha RIB na kwa sasa, tunafanya ufuatiliaji.”

Dk. Nyirahabimana amehamasisha wananchi kutoficha taarifa husika na kuwapachika mimba wasichana.

Suala la wanaume wanaopachika mimba inaonegezeka nchini nzima. Serikali imeanzisha mikakati mabali mbali ili kukabiliana nalo, ila safari ingali ndefu.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.