kwamamaza 7

Wanaodai kodi ya kwa kuchelewa wangali na muda wa kulipa ikiwemo UTC ya Rujugiro

0

Mamlaka ya Mapato ya Rwanda yatangaza kuwa wanaodai kodi kwa inayolingana na kuchelewa wanaweza kulipa hadi mwisho wa mwezi saba, kama anavyotangaza kamishna wa mamlaka hii Richard Tusabe.

Miongoni mwa wanamali hawa wanaodai malipo ya kodi yumo tajiri Tribert Rujugiro Ayabatwa mmiliki wa UTC(Union Trading Center). Tajiri huyu ambae alikwenda uhamisho baada ya kutuhumiwa na serikali kushirikiana na makundi ya wapinzani na mali zake ikiwemo jengo kubwa la UTC lililoko mjini Kigali likashikiliwa na serikali.

Muda si mrefu Mamlaka ya Mapato ya Rwanda iliorodhesha jengo hili kwenye mali zitakazowekwa kwenye mnada iwapo wamiliki wake wakishindwa kulipa kodi hilo kabla ya siku kumi na tano ambazo zilikuwa zimeekewa. Inasemekana kuwa Rujugiro anadai kulipa kodi ambayo ni sawa na 1,100,000,000 ya kipindi kutoka 2007 hadi 2013.

[xyz-ihs snippet=”google”]

La hasha, Rujugiro akijibu haya alionya kwamba mtu ambaye atathubutu kununua jengo lake la UTC kwenye mnada atajuta baadaye kwa kuwa kwa upande wake hadai mtu kodi ila serikalli ililolishika jengo lake inapaswa kulipa kodi kwa sababu shughuli za kibiashara zilizokuwa zikifanyika hapo zinaendelea baado.

Richard Tusabe, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato akiongea na KT Press ametangaza kwamba watu ambao mali zao ziliorodeshwa miongoni mwa zile zenye tishio la kuweka mnadani zimeongezewa muda wa kulipa.

“kukiwa na yeyote ambaye ataonyesha nia ya kulipa tutamrahisisha na aweze kulipa, lakini itakapofika mwishoni mwa mwezi saba tutatekeleza maamzi ya kuweka mali hizo mnadani.

Wadai 13 wengine wa mapato ambao mali zao huenda zikawekwa mnadani ni pamoja na:

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.