kwamamaza 7

Wananchi karibu na mpaka wa Rwanda na Burundi wahofia uwepo wa wanamgambo wanaosema Kinyarwanda

0

Wakazi Wilaya za Mkoa wa Cibitoke, karibu na mpaka wa Rwanda wametangaza kuwa na hofu kutokana na uwepo wa wanamgambo wanaotumia Kinyarwanda katika eneo hili.

Kwa mujibu wa  Radio RPA, kuna tuhumu kwamba hawa wanamgabo ni wa FDLR kutoka nchini DR Congo.

Kutokana na hofu, wili iliyopita shule za msingi karibu na mpaka  kama vile Nyamihana, Ngoma na Miremera ziliahirisha masomo baada ya kuwaona wanamgambo hawa wakiwa kwenye mlima wa Rubona, Wilayani Mugina na Ruhororo, Mkoa wa Cibitoke.

Wengi mwa wanamgambo ni vijana, walifika huko tarehe 3 Aprili 2019 na kujaribu kuingia nchini Rwanda lakini wakashindwa.

Kuna taarifa kwamba kulikuwepo vita kati yao na jeshi la Rwanda msituni Nyungwe kisha wakarudi nchini Burundi na kukaribishwa.

Wakazi wamesema kuwa wana hofu kutokana na hivi vitendo vya wanamgambo wanaotoka Burundi na kuingia nchini Rwanda kwa lengo la kuharibu usalama.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.