kwamamaza 7

Wanajeshi wa Rwanda watatu wauawa na wanamgambo wa FDLR

0

Wanajeshi wa Rwanda watatu wamepigwa risasi na kuuawa na wanamgambo wa FDLR kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa hizi zimehakikishwa na Rais Kagame kwenye mazungmzo na waandishi wa habari jana tarehe 14 Disemba 2018.

“ Ni ukweli, siku zilizopita wanamgambo kutoka  DR Congo wachache sana walikuja karibu na mpaka, nafikiri waliwaua wanajeshi wawil ama watatu. Tunakusanya habari kuhusu walikotoka, msaada na mambo mengine.” Rais Kagame amesema

“ Pengine, badhi yao waliuawa.” Ameongeza.

[penci_related_posts taxonomies=”undefined” title=”Habari nyingine” background=”” border=”” thumbright=”no” number=”4″ style=”list” align=”none” displayby=”recent_posts” orderby=”random”]

Rais Kagame amesisitiza haina budi kulinda usalama aslimia mia na kuwa wakazi hawafai kuishi kwa hofu kwa kuwa usalama umelindwa vilivyo.

Kwa upande mwingine, Rais Kagame amesema FDLR inaungwa mkono na makundi mengine kama vile RNC ya Kayumba Faustin Nyamwasa na kuwa kuna mazungumzo yanayotokea katika nchi jirani kwa kuunganisha hivi vitendo.

Pamoja na hayo, Msemaji wa Jeshi la Rwanda, Luteni Kanuni Innocent Munyengango alihakikisha wanamgambo tisa wa FDLR waliuawa katika hivyo vita.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.