kwamamaza 7

Wanajeshi wa Rwanda na wa Burundi waangaliana kwa  jicho kali kwenye mpaka

0

Hewa mbaya imeonekana kati ya Wanajeshi wa Rwanda na wa Burundi Jumatatu wiki hii kwenye mpaka wa hizi nchi mbili kwa jina la Ruhwa.

Kwa mujibu wa taarifa za Sos Media Burundi,  Kikosi cha polisi kwa wajibu wakupambana na maandamano kimewatukanana wanajeshi wa Rwanda waliokuwa katika kazi zao za kulinda usalama karibu na mto wa Ruhwa.

Taarifa hizi zimesema wanajeshi wa Rwanda wamekaa kimya na hawakujibu chochote.

Kwa sasa, wanajeshi wa Burundi wenye vifaa vikubwa vya vita  wameanzisha kituo cha jeshi kwenye vilima mbali mbali katika wilayani Rugombo, Mkoa wa Cibitoke.

Jambo hili limezua hofu katika wakazi wa haya maeneo. Mmoja mwa wakazi amesema “  Usiku tumeona wanajeshi wengi wakiwa pamoja na Imbonerakure. Tumewaza ni chanzo cha vita.”

Wakazi wameongeza kwamba wameoana magari mengi ya miongoni mwa wanajeshi wa vyeo vya juu yakielekea maeneo ya mpaka wa Ruhwa.

[penci_related_posts taxonomies=”undefined” title=”Habari nyingine” background=”” border=”” thumbright=”no” number=”4″ style=”list” align=”none” displayby=”recent_posts” orderby=”random”]

Wakazi Wilayani  Camakombe na Gitumba wamehofia kuendelea na kazi zao za kulima juu ya hofu ya hali hii kati ya jeshi la Rwanda na Burundi.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.