kwamamaza 7

Wanajeshi wa Rwanda na Burundi waangaliana kwa jicho kali kwenye mpaka

0

Taarifa kutoka nchini Burundi ni kwamba wanajeshi wa Rwanda na Burundi jumapili waliangaliana kwa jicho kali  karibu na mto wa Ruhwa kwenye mpaka.

Wakazi wa maeneo ya Camatoke Wilayani Rugombo na Rugombo Wilayani Mugina amabko ni karibu na mpaka wa Rwanda na Burundi wamesema tangu siku hiyo wanaishi kwa woga wingi kutokana na kutoelewana kati ya wanajeshi wa hizi nchi mbili kama inavyohakikishwa na taarifa za SOS Media Burundi.

Mmoja wa hawa wakazi amesema” Wakazi walikuwa karibu kuanza kukimbia kutokana na hali hii. Haya yakiendelea nitaukimbia huu mji”

Kuna taarifa kwamba kutoka juma pili wanajeshi wa Burundi wameanzisha kituo cha jeshi huko.

Mmoja mwa wanajeshi wa Rwanda karibu na mpaka ametangaza suala hili likiendelea vilivyo watatafuta suluhisho nyingine.

“ Wakiendelea tutatafuta mbinu nyingine za kutoa suluhisho”

Hata hivyo, hizi taarifa hazikutangaza ni upande upi ambao ni chanzo cha hali ya usalama karibu na mpaka kuwa mkia wa mbuzi.

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.