kwamamaza 7

Wanajeshi wa Burundi na Polisi wakaa tahadhari kwa wingi karibu na mpaka wa Rwanda

0

Wanajeshi wa Burundi, Polisi pamoja na Imbonerakure ( vijana wa chama tawala,CNDD-FDD) wamefika kwa wingi karibu na mpaka wa Rwanda.

Kwa mujibu wa taarifa za SOS Media Burundi, hawa  wanachunga usiku na mchana hali ya  usalama katika maeneo  karibu na mto wa Ruhwa, mlima wa Ruhwa Wilayani Rugombo, eneo la Ruce na  Camakombe Wilayani Mugina.

Hizi taarifa zinaeleza kwamba ulinzi huu mkali unalenga kujianda vilivyo kupambana na mashambulizi kutoka Rwanda saa yoyote.

https://swahili.bwiza.com/wanajeshi-wa-rwanda-na-burundi-waangaliana-kwa-jicho-kali-kwenye-mpaka/

Mkazi wa Ruce amehakikisha hizi taarifa kwa kusema “ Usiku kunakuwa Imbonerakure ambao wanazunguka kila pahali wakiwa na bunduki. Wametutaka tusirejee nyumbani juu ya saa mbili usiku kwa kuwa walikuja huku kwa ajili ya kulinda usalama wetu”

“ Yeyote atakayefanya kinyume na hii amri atakuwa mpinzani wa serikali” Mkazi ameambia SOS Media Burundi.

Ulinzi huu mkali umeanzishwa baada ya Rais Nkurunziza tarehe 8 Octoba 2018 alipokuwa Wilayani Butihinda kuwaomba wanausalama kutolegeza.

Nkurunziza alisema hadharani  kwamba mashambulizi yote yanayotokea kasikazini mwa Burundi  yanatoka nchini Rwanda.

Hata hivyo, Rwanda haijafunguka lolote kuhusu madai ya Rais Nkurunziza.

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.