kwamamaza 7

Wanafunzi wahimizwa kupambana na itikadi ya mauaji ya kimbari

0

Tume ya kupambana dhidi ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda (CNLG) imeomba wanafunzi wa shule za sekondari katika wilaya ya Nyagatare kuchangia katika mapambano dhidi ya itikadi ya mauaji ya kimbari. Mwito ulitolewa na mwakilishi wa CNLG tarehe 20 Oktoba 2016.

Zaidi ya wanafunzi 1200 walipewa maelezo juu ya itikadi ya mauaji ya kimbari, namna ilifanyika. Walikumbushwa tena kwamba kuna sheria za kuaadhibu wanaoonyesha hadharani itikadi hio.

Baada ya kuelezewa, wanafunzi waliapa kufuatilia maonyo na kuomba tume hii kuwasaidia na kuwapatia masomo hayo mara nyingi ili kuelewa zaidi historia ya Rwanda hasa hasa mauaji ya kimbari yalifanyika mnamo 1994 dhidi ya Watutsi.

[ad id=”72″]

Miongoni mwa swali ambazo vijana-wanafunzi hujiuliza ni uhusiano kati ya kifo cha rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana na mauaji ya kimbari; mchango wa nchi ya Ufaransa katika mauaji ya kimbari nkd.

Katibu mtendaji wa CNLG, Dkt Jean Damascene Bizimana alisema mnamo mwezi Juni kwamba kuna sura na mbinu mpya zilizojengwa kwa shabaha la kutetea mauaji ya kimbari. Alisema,“Siwezi kusema kuwa hawana akili ingawa wana akili ya unyama, tutawaita wakatiri, tunapashwa kuwafukuza, wana huzuni ya kuwa wameshindwa kufikia kwenye lengo lao, ndiyo maana wanaendelea kusambaza itikadi ya mauaji ya kimbari”.

[ad id=”72″]

Vijana wengi huonyesha kutoelewa historia ya Rwanda hasahasa kuhusu mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yaliyopatikana mnamo 1994. Siku zilizopita itikadi ya mauaji ya kimbari ilijitokeza mashuleni ijapokuwa imepunguzika kulingana na uhamasishaji wa tume mbali mbali za kupambana na mauaji ya kimbari na kuwasaidida waathirika.

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.