kwamamaza 7

Wanafunzi wa shule za msingi walazimishwa kutotumia ujanja katika mtihani wa taifa

0

Wanawafunzi wa shule za msingi wameanza leo mtihani wa taifa wa kufunga mwaka wa 2016. Wizara ya elimu nchini Rwanda inasema kwamba wanafunzi waliongezeka kulingana na mwaka uliopita katika shule za msingi na kupunguzika katika shule za sekondali.

Katika ujumbe wake kwa uzinduzi wa kufanya mtihani wa taifa ulifanyiwa katika shule la msingi la St. Famille mjini Kigali, Isaac Munyakazi ambaye ni waziri wa serikali kuhusika na elimu ya shule za msingi na sekondari katika wizara ya elimu, aliwalazimisha wanafunzi kutodanganya na kutotumia ujanja wakati wa mtihani.

[ad id=”72″]

Tabia ya kudanganya na kutumia ujanja katika mtihani wa taifa husemekana kujitokeza hasa hasa katika shule za mjini, ijapokuwa waziri Munyakazi alithibitisha kwamba walitia bidii kuepuka jambo hili kujitokeza na kuaadhibu watakaokamatwa.

img_9169
Wanafunzi husakwa kabla ya kuingia katika chumba cha kufanyia mtihani

“Walivyosema mithili ya kudanganya au ujanja katika mtihani, nilisema kuhusu hivi kabla na natumai kuwa hakuna mmoja atakayekamatwa akifanya kitendo hiki. Tumejitaarisha pamoja na polisi kuzuia kitendo hicho cha kudanganya na kutumia ujanja katika mtihani wa taifa na kuwaadhibu wenye hatia watakaogunduliwa,” Waziri alisema.

Kwa upande mwingine kuna wanafunzi ambao wamezuiliwa kufanya mtihani kwa sababu tofauti mithili ya kukosa nidhamu baada ya kujaza faili ya kufanya mtihani na wengine waliacha shule.

[ad id=”72″]

Mtihani wa taifa wa shule za msingi hufanywa katika siku tatu. Wanafunzi walishiriki mtihanini mwaka uliopita wa 2015 walikuwa 168,290 kinyume na 194,679 katika mwaka huu wa 2016. Waliongezeka kwa kiwango cha 16%.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.