kwamamaza 7

Wanachama wa RPF Inkotanyi wa jimbo la mashariki wamchagua Paul Kagame 100%

0

Jumamosi hii ya tarehe 10 Juni, wanachama wa RPF wa Jimbo la mashariki wamejuika katika mkutano mkuu uliofanyika Rwamagama ambapo walikuwa wakimtafuta mgombea wa kusimamia Jimbo la mashariki katika mchakato wa kumtafuta mgombea atakae simamia chama cha RPF kwenye ngazi ya nchi.

Wanachama wote 1261 waliohudhuria mkutano, wamemchagua Paul Kagame.

Kagamba Wilson, ni mjawapo ya waliotoa hotuba wakifafanua jinsi hawana mwingine anaefaa kuingoza Rwanda isipokuwa rais Kagame. Amesema “tumemchagua Kagame kwa kuwa ndie aliekua na mafanikio kuliko wengine, alikuwa kiongozi aliyeonyesha tabia ya kuwapenda wanyarwanda, aliongoza vita vya kuikomboa nchi, alikomesha Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi na kuwarudisha wakimbizi, amewapa wanyarwanda mwelekeo, kwa sasa tuna amani, amewapa wanawake fursa ya kuchangia katika shughuli za nchi, ameipa Rwanda heshima kimataifa, ni mgombea anayeshtahili kuingoza Rwanda..

[xyz-ihs snippet=”google”]

Utawala bora na vitendo vya kimaendeleo ndivyo vilifanya raia wa jimbo la mashariki kutoka ngazi ya kijiji kumchagua Kagame kama mgombea wao kama alivyoadokeza Myenyekiti wa chama cha RPF kwenye ngazi ya Jimbo la Mashariki, Kanzayire Judith.

Alisema “ tumependa kumchagua Paul Kagame kwa ajili ya utawala bora aliowaletea wanyarwanda, jimbo hili lina maendeleo kadha ikiwemo kuwaletea wanachi maji safi, na kwa kuwa jimbo letu lilikumbwa na tatizo la ukame na walitusaidia pia kumwagilia maji kwenye mimea na kuisaidia mifugo kupata maji, inaeleweka raia walitilia maanani mambo mengi na wakamchagua mtu ambaye wanaimani ataendelea kuwaletea maendeleo ya kujali ustawi wa maisha yao”

Alieendelea kusema kuwa ndio sababu walimchagua Kagame100%

Shughuli za kutafuta atakaekuwa mgombea urais wa upande wa RPF zinaendelea kutoka ngazi za vijiji nchini kote, ambapo Inaonekana kuwa rais wa jamhuri, Paul Kagame hana mshindani mwingine

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.