Swahili
HABARI MPYA SIASA

Wanachama wa FDU-Inkingi wanaotuhumiwa vitendo vya ugaidi wasimama kizimbani

Wanachama wa FDU-Inkingi wakiwemo kiongozi makamu wa kwanza,Boniface Twagirimana na meneja wa fedha,Gasengayire,Janvier Twagiramungu wamefika mahakamani ili kufafanua kuhusu shutuma za kuunda kundi la kijeshi kinyume na sheria na kudhamiria kutenda maovu kwa serikali ya Rwanda.

Kiongozi makamu wa kwanza wa chama cha FDU-Inkingi,Boniface Twagirimana

Mahakamani tarehe 22 Septemba 2017,Boniface Twagirimana akijibu swali la hakimu kuhusu matumizi ya fedha zinazotoka ugenini ameleza kwamba meneja Gasengayile hajui mengi kuhusu fedha hizi kwani mara nyingine anakuwa gerezani  na kuwa anazojua matumizi yake ni zile za kumsaidia kiongozi wa chama,Ingabire Victoire aliye gerezani.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kwa mujibu wa taarifa za radiyo ya sauti ya marekani,Mmoja wa wanasheria Me Anoinette Mukamusoni akieleza swali la hakimu kuhusu fedha hizi ameleza kwamba ikiwa serikali haitaki chama kupokea fedha za ugenini,haina budi kuweka bajeti ya kuwasaidia na kuongeza kwamba ushahidi wa washtakiwa hauna thamani kulingana na sheria kwa kuwa waliteswa kimwili kama vile kufungiwa mahali wasipojua, kuvaa mapingu siku nzima,madai yanayokanwa mno na mwendesha mashtaka.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Upande wa uendesha mashtaka umeombea washtakiwa kufungwa mwezi mzima,fikra anazopinga sana mwanasheria Me Gatera Gashabana kwa kueleza kwamba mahakama haina budi kuwachia huru washtakiwa kwa kuwa mahakama ilifuta shutuma za Ingabire Victoire zilizokuwa sawa na za washtakiwa hawa.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Uamuzi wa mahakama utajulikana tarehe 26 Septemba 2017.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com