Swahili
Home » Wanachama wa FDU-Inkingi wanaotuhumiwa vitendo vya ugaidi wafungwa mwezi kizuizini,mmoja achiwa huru.
HABARI MPYA SIASA

Wanachama wa FDU-Inkingi wanaotuhumiwa vitendo vya ugaidi wafungwa mwezi kizuizini,mmoja achiwa huru.

Wanachama nane wa FDU-Inkingi wakiwemo kiongozi makamu wa kwanza,Boniface Twagirimana na meneja wa fedha,Gasengayire wamehukumiwa kufungwa mwezi kizuizini na kumuachia huru,Janvier Twagirayezu kwani hana hatia.

Kiongozi makamu wa kwanza wa chama cha FDU-Inkingi,Boniface Twagirimana

Kwa mujibu wa taarifa za radiyo ya sauti ya marekani,Mahakama kuu ya Nyarugenge imeleza kwamba watu nane  wanastahili kufungwa mwezi kizuizini kwani kuna kuwa sababu maalum za kwatuhumiwa.

 Uendesha mashtaka ulieleza kwamba hawa waliunda kundi la kijeshi la kupindua serikali ya Rwanda kwa jina la P5 yaani RNC, PDP-Imanzi,FDU-Inkingi,PS-Imberakuri kupitia wanamgambo wa FDRL.

Kwa kutegemea ushahidi wa Mathias Ndayishimiye na Norbert Ufitamahoro waliokubali kuwa na hatia, mahakama imeamua kwamba inaonekana kwamba hawa watu nane wanatuhumiwa na shutuma za mambo ya ugaidi.

Baada ya kutangaza hukumu,watuhumiwa wamekata rufaa ya uamuzi huu.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com