Swahili
Home » Waliokimbizwa kutoka Tanzania wanajivunia maendeleo chini ya Utawala wa Kagame
HABARI

Waliokimbizwa kutoka Tanzania wanajivunia maendeleo chini ya Utawala wa Kagame

Anajivunia maisha mazuri

Wananchi wa Nyamasheke tarafa ya Karambi wa mtaa wa Rushyarara wanamshkuru rais Kagame kwa kuwa amewarudishia heshima kwa kuwa aliwasaidia kupata makazi, mashamba na hata ng’ombe.

Wananchi hawa wanajumwika katika familia 18 ambao walikimbizwa kutoka nchi ya Tanzania na wakarudi mikono mitupu lakini wanasema Paul Kagame aliwasaidia kujikwamua na matatizo hayo licha ya kuwa walitua Nyamasheke wakiwa ni mara ya kwanza kupafika.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hata hivyo walisaidiwa kupata makazi, wakapewa ng’ombe kupitia mfumo wa Girinka na maziwa kwa sasa wanakunywa bila tatizo lolote, walipewa mashamba na wanalima wakapata mazao.

Mukamusoni Léocadie ambaye anasema alikuwa katika hali ya mbaya anasema alikimbizwa kutoka Karagwe ya Tanzania ambapo ndipo alipozaliwa lakini kwa sasa anasema ni mfugaji wa kuigwa.

“kwa sasa niko mfugaji mkali kwa kusaidiwa na Paul Kagame. Alitupa makazi, alitupa kila kitu, familia zetu 17 kwa  18 zilipewa ng’ombe kupitia mfumo wa Girinka, maziwa tunapata, na rutuba yakutuezesha kupata mazao mengi, tuna siha njema kwa sasa, tuna simu za mikononi na nadhani watoto wetu wa kizazi cha kesho wataishi raha mstarehe wakiwa wanaishi kwenye chimbuko lao”

Mukamusoni aliendelea kusema kwamba wanamshkuru sana Kagame aliyekubali kuwapokea tofauti na serikali ya wakati uliopita iliyokuwa ikiwakatalia kurudi wananchi wake waliokuwa wakiishi uhamishoni. Na kwa hivyo wataendelea kumwunga mkono.

Niyitegeka Jerôme Katibu mtendaji wa tarafa hiyi ameiambia Bwiza.com kwamba wananchi hawa wana maisha mazuri na kwamba hali yao inafuatiliwa kwa karibu na hata ng’ombe walizopewa zilianza kuzaa na wameanza kuwapa wenzao na kwa hivyo anawashkuru kwa mchango wao wakushirikiana na wananchi wengine katika shughuli za nchi.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com