Wanajeshi wa Rwanda wanaolinda amani nchini Sudani Kusini katika misheni ya umoja wa kimataifa (UNMISS) walipewa heshima kwa kazi imara walifanya juzi, 15 Disemba 2015.

Kamanda wa wanajeshi wa UNMISS, Major General Chaoying Yang alisifu wakati wa sherehe mjini Juba, ubingwa wa Rwanbatt-1 na ushuja wa kuwalinda raia nchini Sudani kusini.

Chaoying alisema, “Ni furaha yangu, kwa niaba ya katibu mkuu wa Umoja wa kimataifa (UN), Ban Ki-Moon, ya kuwapatia tuzo nyinyi nyote kama heshimu ya kazi ya kitalaam mlifanyia Sudani kusini.”

Alieleza zaidi kwamba wakati vita vilimalizika mnamo 2013, wanajeshi kutoka Rwanda walisaidia UNMISS na kujiamini katika kazi za kuwalinda raia na kusaidia wengine kufikia lengo za UNMISS.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Kuhusu mchango wa jeshi la Rwanda katika mashambulizi ya Julai, Jenerali yang Chaoying alisema; “katika mapambano yaliyopita mnamo mwezi Julai, mlishinda kwa kuwalinda mamia ya raia walipokuwa wanataka mahali pa usalama katika makao ya UNMISS ya Tomping,…mlionyesha uwezo na jitihada za kutekeleza misheni ya kuwalinda raia walipoogopeshwa na ukatili katika sehemu ya Equatoria.”

????????????????????????????????????

 

Tangu mwaka wa 2014, nchi ya Rwanda ilitoa msada madhubuti katika misheni za kulinda amani hata katika Umoja wa kimataifa na umoja wa Afrika. Rwanda ilikuwa ya kwanza miongoni mwa nchi kuwatuma wanajeshi katika misheni ya UNMISS tangu 2011.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.