Home HABARI MPYA walemavu wahamasishwa kuachana na tabia ya kuombaomba
HABARI MPYA - Uncategorized - December 5, 2016

walemavu wahamasishwa kuachana na tabia ya kuombaomba

Wizara ya serikali za mitaa imewaita walemavu kuhifadhi heshima yao na kuachana na tabia za kuombaomba barabarani.

Mwito ulitolewa na waziri wa serikali za mitaa Francis kaboneka, alipohudhuria sikukuu ya kimataifa ya kukuza haki za walemavu; iliyoshirikiwa kitaifa katika wilaya ya Rwamagana mnamo tarehe 3 Disemba 2016.

“Vinaonekana kama tungali na walemavu ambao huombaomba. Ningependa kuwaita walemavu na viongozi wao pamoja na shirika nyingine kuwahamasisha walemavu wanaofikiri kwamba kuwa na ulemavu ni kupoteza heshima. Kuombaomba ni tabia mbaya.” Waziri kaboneka alisema.

dscn0371
Walemavu wamelalamika kwa kutopata msada wa serikali

Ijapokuwa kuna miradi tofauti ya serikali na shirika binafsi inayowasaidia walemavu, kuna wengi (Walemavu) ambao husema kwamba hawajapata kitu maluum cha kuwasaidia ingali ni fukara; kwa hiyo hujitokeza barabarani kuomba ili kuendeleza maisha.

[ad id=”72″]

Akimana anayeishi waliyani Rwamagana alisema, “Sina mikono pia nakuwa fukara, lakini sijapata usaidizi wowote kutoka serikali au shirika binafsi. Maisha yangu na watoto wanne yanategemeana na kuomabaomba. Nitaishi namna gani kama wanapiga marufuku tabia ya kuombaomba?”

Kila mwaka tarehe 3 Disemba, tangu mwaka wa 1992; dunia nzima hushirikia sikukuu ya walemavu. Sikukuu hii huwa na lengo maluum ya kuelewa tatizo za ulemavu, kutoa msada kwa walemavu na kuhifadhi ustawi wa walemavu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Theogene U @Bwiza.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.