kwamamaza 7

Wakimkuta Kagame wajumbe wa Kamati ya Wayahudi Wa Marekani wasema watakua watetezi wa Rwanda

0

Tarehe 29 Juni 2017 ndipo Rais Kagame alipowapokea jana wajumbe wapatao 20 wa Kamati ya Wayahudi wa Marekani(AJC) ambao wamekuwa katika ziara ya siku nne

Eliseo Neuman, ambaye ni mkuu wa Taasisi ya Afrika kwenye Kamati ya Wayahudi wa Marekani,akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya wajumbei alisema kwamba ziara hiyo nchini Rwanda ilikuwa na madhumuni ya kuchunguza fursa za biashara na kuulewa kwa kina muungano wa kihistoria uliyoko kati ya Wanyarwnda na Wayahudi. Habari kutoka The New Times yasema.

Stanley M. BergamanStanley M. Bergaman, mwanashirika wa AJC na Kiongozi Mtendaji wa Henry Schein, chuo cha marekani cha biashara kutoa vifaa na madawa vya kutibu, meno na hata mifugo, amesema amevutiwa na mazingira ya kibiashara na hata fursa zilizoko ambazo nchi hii yaijazitumia.

“ tumeona kwamba Rwamda ingeweza kuwa mahali panapofaa kuendesha biashara, serikali iko na nia ya kusaidia na iko aminifu, ni mahali salama, penye usafi na watu wafanyakazi wenye elimu. Hapa ni mazingira mazuri ya biashara,” Bergaman asema

“ tuko kwenye juhudi za kuanza shirika la kuendeleza biashara kati ya Kamati ya Wayahudi na Marekani na Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Akiongea kuhusu historia sawa ya mauaji ya Kimbari ambayo nchi hizo mbili zimepitia, Bergaman amesema kwamba kikosi chao kimeshangazwa sana na jinsi Rwanda ilivyojiepusha na historia mbaya iliyopitia na kuunda nchi ya umoja.

Amesema zaidi kwamba urafiki kati ya AJC na Rwanda utazaa sauti za kutetea wanaokana na kupuuza mauaji ya kimbari ulimwenguni.

“Tunahistoria sawa Lakini tulichoweza kugundua katika ziara yetu ni kwamba, Rwanda si nchi tunayo historia ya pamoja tu bali ni nchi iliyoweza kutokea mbali na kujiendeleza,” asema Bergaman

“si nchi nyingi zilizoweza kuyafikia haya ambayo rais Kagame na raia wa Rwanda waliweza kuyafikia. Ni historia ya kusifiwa na mna rafiki Marekani watakao tetea Rwanda” aliongeza

Waliwakuta viongozi wengi katika kipindi cha ziara yao ambao mojawapo ni waziri wa mambo ya nje Louise Mushikiwabo, Kiongozi mkuu mtendaji katika Idara ya Rwanda ya Maendeleo Clare Akamanzi, na viongozi wengine kutoka Tume ya Taifa ya Kupambana na Mauaji ya Kimbari.

Kikosi cha waakilishi hawa kilizuru pia Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali kwa ajili ya kuwapa heshima waathirika wa Mauaji ya Kimbari dhidi ya watutsi ya 1994.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.