Shirika la kimataifa linaloshughulikia maswala ya uhamiaji IOM limethibitisha. Zaidi ya wakimbizi 30 kutoka Somalia walioko Yemen wameuawa katika shambulio lililolenga boti waliokuwa wakisafiria wakiwa kwenye bahari ya Shamu.

Vikosi vinavyoshughulikia doria za baharini katika bandari ya Hodeidah inayodhibitiwa na waasi Wa-houthi vinasema boti hilo lilikuwa linatoka Yemen kuelekea Sudan wakati liliposhambuliwa kwa kombora.

Kituo cha habari kinachomilikiwa na waasi hao kimedai shambulio hilo limefanywa na ndege ya helikopta aina ya Apache .

Zaidi ya majeruhi 80 wa mkasa huo wamekimbizwa hosptialini.

Eneo la Hodeidah ni mojawapo linalokumbwa na mashambulio ya mara kwa mara kutokana na mzozo wa kivita unaoendelea baina ya jeshi la Yemen linaloungwa mkono na lile la Saudia, dhidi ya waasi hao wa Houthi wanaopinga serikali ya Yemen.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

[xyz-ihs snippet=”google”]

Leki@bwiza.com

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina