Swahili
Home » Wakimbizi waliotoka nchini Israel washauri wenzao waliobaki kutokuja nchini Rwanda
HABARI MPYA

Wakimbizi waliotoka nchini Israel washauri wenzao waliobaki kutokuja nchini Rwanda

Wakimbizi kutoka Israel waliohamia nchini Rwanda wameonya wenzao waliobaki kutokuja nchini Rwanda.

Taarifa za Haaretz zimeeleza kuwa hawa wakimbizi wameonya wenzao hili kutokana na kuwa hawakuweza kupata waliyokuwa wakitarajia yaani maisha mazuri.

Mmoja wao asili ya Eritrea, Goitom, 28, wiki hii alitangazia Haaretz mjini Kigali kwamba maisha yake nchini Rwanda ni kama “kuishi gerezani”

Goitom amesema”Sikutaka kuenda gerezani,nirifikiri kwamba ni vizuri kuenda nchini Rwanda lakini hapa ni yale yale”.

Huyu amesema kuwa anaishi katika hali mbaya bila makazi,chakula na kazi kwa kuwa waliokuwa wakimusaidia walikoma.

Ameogeza kwamba kuna siku ambayo analala njaa na kuwa alipata hasara alipoanzisha duka dogo la kuuza bidhaa kwa kuwa hakujua lugha ya Kinyarwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Taarifa hizi zimesema kwamba nchini Rwanda kunabaki wakimbizi tisa tu kutoka  Israel.

Pamoja na haya Rais wa Rwanda,Paul Kagame alipokuwa mjini Davos,Switzerland kwenye mazungumzo na waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu waliamua kwamba wakimbizi watatumwa nchini Rwanda kufuatia sheria za kimataifa.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Izindi wakunda

Tanga Igitekerezo

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Bwiza.com