kwamamaza 7

Wakimbizi wa Rwanda huko Zimbabwe wakisikia neno kurudi kwao wanaumwa sikio

0

Wanyarwanda wanao ishi katika kambi la Tongogara huko Zimbabwe, walionyesha wazi kwamba hawafurahiye wanayo ombwa na serikali ya Zimbabwe pamoja na jamii ua umoja wa mataifa wanao husika na wakimbizi UNHCR, wakiombwa kurudi Rwanda.

Prisca Mupfumira, waziri wa kazi alisema kwaba wakimbizi hao hawataki kurudi Rwanda na haikuwa maamzi ya Zimbabwe pekee ya kuwajesha.

Eti: “Haiko serikali ya Zimbabwe iliamua ili wakimbizi wa Rwanda kurejea kwao, ni mpango ulio toka katika mkutano wa Geneva mwaka wa 2016 kuhusu kuwarejesha wakimbizi wote Rwanda mahali walipo dunia nzima”.

Mmoja wa wakimbizi wa Rwanda huko Zimbabwe alisema kwamba wanahuzunikishwa na kuwa wanakwenda kurudishwa Rwanda na kusema kwamba hawapo tayari na wengine wakisema hawafurahi kwa sababu  wapo na mali yao huko.

Serikali ya Zimbabwe inaomba hao wanyarwanda kurudi kwao kwa kuwa Rwanda inaomba Wanyarwanda wote wanao ishi nchi zingine kurudi katika nchi ya ukoo hadi tarehe 31 Disemba 2017, atakaye vukisha tarehe hio hataitwa tena mkimbizi.

Wakimbiziz wa Rwanda wanao ishi Zimbabwe ni zaidi ya 500, wengi wao walikimbia mwaka wa 1994 wakikimbia mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi.

Tangu 2002 serikali ya Rwanda iliomba mataifa kuwaleta wakimbizi wa Rwanda kwa sababu walicho kikimbia kimekwisha.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Wizara kuhusika (MIDMAR) ikishirikiana na  UNHCR, wanampa msaada kila mkimbizi anaye rudi kwa makusudi yake dolla 250 ya marekani mtu mzima, mtoto akipewa dolla 150 hesabu ambazo huonyeshwa na UNHCR (2016) ikionyesha kuwa Wanyarwanda ambao wangali ukimbizini ni wapatao 286.336.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Leki/bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.