kwamamaza 7

Wakimbizi kutoka Burundi watoroka Kambi ya Mahama

0

Asubuhi ya tarehe 15 Juni 2017, Polisi ya Burundi imetangaza kwamba kuna wakimbizi 13 waliokuwa wametoroka kambi ya Mahama iliyoko Rwanda, na wakazuiwa kuvuka na Polisi ya Rwanda wakiwa mpaka wa Gasenyi-Nemba ukiingia Jimboni Kirundo.

Wakimbizi hawa waliingia nchini mwao jioni ya Ijumaa ya wiki jana. Askari polisi wa Polisi ya Rwanda waliwakatalia kuingia na wakapanga njama na kuwatoroka. Wanawake wawili waliokuwa na watoto 6 ndio waliowahi kuongea na vyombo vya habari kwa mjibu wa Sauti ya Amerika na kueleza sababu waliyoamua kutoroka kwa faragha.

“Tulitoka hapo kambi ya Kirehe ya Rwanda kwa kuwa tulikuwa na matatizo ya malezi ya watoto wetu na tulipofika mpakani tulizuiwa na polisi ya Rwanda, ilipofika saa mbili za jioni tuliwachunga na tukavuka mpaka kwa kutoroka” Murerwa Venantie alisema

[xyz-ihs snippet=”google”]

Bi huyu anaendelea kusema kwamba walizuiwa na polisi ya Rwanda kwa sababu hawakuwa na vitambulisho kama wakimbizi na walitaka warudi kwenye kambi.

Licha ya wanawake hawa 2 na watoto wao sita kulikuwa na watu wengine waliokuja kwa kuwafuata na wakapitia kwanza kujieleza mbele ya viongozi wa wakimbizi kabla ya kuruhusiwa kwenda.

Sauti ya Amerika ilisema kwamba miongoni mwa wale waliopitia kwa viongozi kulikuwemo na mwanamke mwenye watoto 4, ambaye aliambia sauti ya Amerika kuwa aliweza kuvuka mpaka kwa urahisi kwa kuwa alikuwa na hati ya wakimbizi. Na alisema kwamba walioshurutishwa kurudi ni wenye kutokuwa na vitambulisho.

Polisi ya Burundi kwa kujibu haya ilisema kwamba hii ni ishara kwamba wakimbizi walioko Rwanda wanashikiliwa kama wafungwa.

“Inaonekana kuna warundi wengi wanaotaka na wa kataliwa kurejea kwao na Polisi ya Rwanda ” amesema kamishna wa Polisi Jacques.

Alisema pia kuwa haelewi sababu Warundi wanayokataliwa kurejea kwao. Amendelea kusema kwamba polisi ya Rwanda ingearifu polisi ya Burundi na ikafuatilia hali ya mambo inapoona kuna Warundi wanao nia ya Kurejea kwao.

Warundi hawa walikutana wenzao 82 waliokuwa mpakani wakiwa wameshurutishwa kurejea kwa kwa sababu ya kutokuwa na vitambulisho.

Hii ni idadi zaidi ya Warundi 92 ambao walilipotiwa kurejea kwao kwa sharti na serikali ya Rwanda katika wiki iliyopita.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.