kwamamaza 7

Wakimbizi asili ya Rwanda wakataa kuhamia Rwanda

0

Wakimbizi asili ya Rwanda  wametuma  barua kwa  shilika la kimataifa la kuhudhumia wakimbizi(UNHCR) wakiwasilisha ombi  kwamba hawatahamia nchini Rwanda hata kama hadhi ya ukimbizi kwa Wanyarwanda ilikomeshwa mwisho wa mwaka jana 2017.

Mmoja wao Memory Mugisha, ambaye ni mkimbizi nchini Marekani ametangaza kwamba wamekataa jambo hili kwa kuwa hawana matumaini ya usalama wao watakapohamia nchini Rwanda.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mugisha ameteta” serikali ya Rwanda inalenga kuwadhibu wale watakaorudi nchini”.

Taarifa za chombo cha habari Malawi24 zinasema kwamba ombi la hawa wakimbizi linaeleza kwamba wale waliohamia nchini Rwanda walitekwa nyara na maafisa wa usalama na kuwa waliokimbilia nchini jirani waliuawa ama kutekwa.

Juu ya haya,serikali ya Rwanda ilianzisha mpango wa jina “Come and See, Go and Tell in 2013” yaani kuja na kuona,nenda kawaambie   wenye lengo la kuhamasisha wakimbizi asili ya Rwanda kurudi kwao.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.